This website uses cookies. To read more about our Privacy Policy, click here.

#PeoplesVaccineKE ni kampeni ya ulimwenguni pote kushinikiza usambazaji wa bure na ufikiaji bila masharti kwa chanjo ya COVID-19.

Tunaamini kwamba chanjo ya COVID-19 inapaswa kutambuliwa kama faida ya umma na ufikiaji unapaswa kuwa kwa masilahi ya watu wote kila mahali, sio wale tu ambao wanaweza kuimudu.

homepage peoplesvaccine image

Lengo la kampeni hii ni kuhakikisha mtiririko wa bure na upatikanaji wa chanjo ya COVID-19. Mahitaji haya yamewekwa kuunda utaratibu unaolengwa na jamii kuhakikisha kila mmoja wetu anaweza kupata chanjo bila malipo au masharti, kila mahali ulimwenguni na kujifunza kutoka kwa wanaharakati wa 'chanjo ya watu' (People’s vaccine) ulimwenguni kote, kwa nguvu na lazima tuutekeleza hatua hizi nchini Kenya.

Tunakusudia kuimarisha jamii zetu zote na kuhakikisha kuwa chanjo hii sio tu kwa jamii ya kisiasa, wasomi na wale ambao wanaweza kuitunukia, inapaswa kuwa ya kila mtu ilhali ya cheo.

MATAKWA YETU

Hatua za haraka za utekelezaji wa Chanjo endelevu ya wote nchini Kenya

Sisi waKenya tunadai kuwa mara chanjo ya COVID-19 itakapopatikana:

1

Wakenya lazima wafahamishwe kupatikana kwa Chanjo ya COVID-19 na mara tu inapopatikana ndani ya mipaka ya Kenya.

Serikali ya Kenya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, lazima ikubali hadharani na kushiriki habari yoyote muhimu na habari za kupatikana kwa chanjo ya COVID-19 na iko ndani ya mipaka ya Kenya

2

Chanjo inapaswa kuwa BURE kwa Wakenya wote.

Serikali ya Kenya haipaswi kuweka bei kwenye chanjo ya COVID-19. Utengenezaji wa chanjo ya COVID-19 kwa kuweka dhamana ya kifedha juu yake kutawatenga maelfu ya Wakenya kuipata kutokana na ufinyu wa kifedha.

3

Chanjo inapaswa kupatikana kwa Wakenya wote katika kaunti zote 47.

Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Afya, inapaswa kuweka utaratibu wa vitendo na wa kuaminika wa kuruhusu chanjo kutawala kwa kaunti zote 47 na sio kuzuiliwa tu ndani ya Nairobi. Wizara ya Afya na wadau husika wanapaswa kuunda na kutenga kila kaunti na vituo vya kliniki vya muda, vinavyohama na wafanyikazi wa huduma ya afya wenye vifaa vya kutosha kutoa chanjo kwa wakaazi wote kwa eneo tofauti tofauti. Kwa upande mwingine, serikali inapaswa pia kutekeleza chanjo ya mlango kwa mlango kwa wale ambao hawawezi kuondoka majumbani mwao kwa sababu tofauti. Chanjo lazima ipatikane kwa Wakenya katika kila sehemu ya Kenya.

4

Wafanyakazi wa huduma za kiafya wa mbele na wafanyikazi wa karibu hospitalini lazima wapewe kipaumbele katika kupata chanjo ya COVID-19.

Hii ndio kidogo serikali ya Kenya inaweza kufanya baada ya kuiba na kusimamia vibaya pesa ambazo zilipaswa kuhakikisha ulinzi wa wafanyikazi wa huduma ya kiafya na kupambana na COVID-19 Kenya, kuhatarisha maisha ya wafanyikazi wa huduma za kiafya na wafanyikazi wa hospitalini.

5

Serikali ya Kenya lazima ihakikishe ufadhili wa umma uliotengwa kwa chanjo ya COVID-19 ni wazi na kuhakikisha uwajibikaji kwa Wakenya kwa jumla.

Serikali ya Kenya lazima ifanye shughuli zote zinazofanywa kuhusu chanjo ya COVID-19 nchini Kenya kuwa wazi na kupatikana kwa raia wa Kenya. Wakati wote wa janga hili la COVID-19, Wakenya wameona kuongezeka kwa unyanyasaji, usimamizi mbaya, ufisadi na wizi wa fedha za misaada za COVID-19 zilizokusudiwa Wakenya.

6

Serikali lazima ishirikishe mashirika ya wanaharakati wa kimsingi na kijamii, na washirika, kuelimisha na kuongeza uelewaji wa chanjo hiyo katika jamii zetu zote kitaifa.

Katika kesi hii, serikali inastahili kufanya kazi na wafanyikazi wa jamii nchini, lazima ielimishe na kwa pamoja kuongeza uelewaji wa chanjo ya COVID-19 na kuondoa maoni potofu au ‘disinformation’ kuhusu chanjo. Kwa upande mwingine Wizara ya Afya inayofanya kazi na wataalamu wa afya inapaswa pia kutumia majukwaa haya kuelimisha raia juu ya athari mbaya za chanjo kwenye miili yetu, kama athari hasi hizi zitakuwepo.

picha iliyoandikiwa hatua za haraka za utekelezaji wa Chanjo endelevu

TIMU

Kampeni hii imewezeshwa na juhudi za hiari na mshikamano wa waandaaji, wanaharakati, watafiti, wakili, wahudumu wa afya na WaKenya wote wanaotarajia chanjo ambayo ni ya bure na inayoweza kufikiwa na wote na kielelezo cha bure na kinachoweza kupatikana tuweze kukusudia na kupigania Dawa kwa wote bila vikwazo.

The PeoplesVaccineKE logo and posters by coconutsakura is licensed under CC BY-NC 4.0creative commons logocreative commons attribution logocreative commons non-commercial logo